Vyakula Bora vya Kuimarisha Kinga ya Mwili kwa Wazee
- ThriveCare Nutrition
- May 5
- 1 min read
Kadri umri unavyoongezeka, kinga ya mwili hupungua, na kufanya wazee kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa mbalimbali. Lishe bora ni msaada mkubwa katika kuimarisha kinga ya mwili kwa wazee.
Virutubisho Muhimu kwa Kinga ya Mwili:
Protini: Inasaidia katika ujenzi na ukarabati wa tishu. Vyanzo bora: maharagwe, dagaa, samaki, mayai.
Vitamini C na E: Zinapambana na uvimbe na kusaidia kinga. Vyanzo bora: mapera, machungwa, mboga za majani.
Zinki: Muhimu kwa ukuaji wa seli za kinga. Vyanzo bora: mbegu za maboga, karanga, dengu.
Omega-3: Hupunguza uvimbe na kuimarisha kinga. Vyanzo bora: samaki wa mafuta kama sato, dagaa.
Mikakati Muhimu kwa Wazee:
Kula angalau mara 3 kwa siku.
Kujumuisha matunda na mboga kwenye kila mlo.
Kunywa maji ya kutosha (angalau lita 1.5 kwa siku).
Epuka vyakula vya sukari na chumvi nyingi na mafuta mengi.
Kwa lishe bora, wazee wanaweza kuongeza uwezo wao wa kupambana na maambukizi na kuwa na maisha marefu yenye afya.
Comments