Kuimarisha Kinga Dhidi ya Kuharisha kwa Watoto Kupitia Lishe
- ThriveCare Nutrition
- Jul 30
- 1 min read
Kuharisha ni moja ya sababu kuu za vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania. Lishe bora inaweza kusaidia kuzuia na pia kuharakisha kupona kwa mtoto aliyeathirika.
Chanzo kikuu cha kuharisha:
Mazingira machafu
Kunywa maji yasiyo salama
Lishe duni na kudhoofika kwa kinga ya mwili
Lishe bora wakati na baada ya kuharisha:
Maji ya kutosha- ORS (maji ya chumvi na sukari), supu ya nyumbani, maji ya nazi
Lishe nyepesi lakini yenye virutubisho- Uji wa lishe (maji mengi), wali mweupe na ndizi, supu ya karoti na viazi
Protini za mmea- Maharagwe yaliyopondwa vizuri au maziwa kwa kiasi
Zinki- Inasaidia kuponya utumbo: karanga, dagaa, uji wa dona
Baada ya kupona:
Rudisha mtoto kwenye ratiba ya kawaida ya chakula polepole
Ongeza matunda na mboga taratibu, kama maparachichi na embe
Watoto wanaopata chakula chenye virutubisho wakati wa kuharisha hupata nafuu haraka na wana kinga bora ya mwili.
Comments