Vinywaji vya Asili vya Kuupa Mwili Joto na Kuongeza Nguvu
- ThriveCare Nutrition
- Jun 27
- 1 min read
Katika kipindi cha baridi, miili ya watoto na wazee huhitaji joto na nishati zaidi. Vinywaji vya asili vinaweza kusaidia kuongeza nguvu bila kemikali au sukari nyingi.
Chaguzi bora za vinywaji vya asili:
Chai ya tangawizi na mdalasini: huongeza joto la mwili na kusaidia mfumo wa upumuaji.
Uji wa lishe wa moto: una wanga, protini na mafuta bora – hufaa kama kifungua kinywa.
Supu ya mboga au kuku: huongeza maji mwilini na kusaidia lishe kamili.
Maziwa ya moto na asali: hutoa nishati na kusaidia kupunguza uchovu.
Vidokezo kwa familia:
Epuka vinywaji baridi au soda kipindi cha baridi – havina virutubisho muhimu na hupunguza joto la mwili.
Tumia viungo vya asili kama pilipili manga, tangawizi na mdalasini kwenye vinywaji.
Watoto wasiozoea chai, wapatie uji wa lishe ulioongezwa karanga na maziwa.
Matumizi ya vyakula na vinywaji vya asili kama sehemu ya ulinzi wa afya kwa msimu wa baridi.
Comments