top of page
Search

Umuhimu wa Mafuta Mazuri katika Kipindi cha Baridi kwa Watoto na Wazee

  • ThriveCare Nutrition
  • Jul 4
  • 1 min read

Mafuta hayapaswi kuogopwa – hasa katika msimu wa baridi ambapo mwili unahitaji nishati ya kutosha. Mafuta ya asili ni chanzo muhimu cha nguvu na husaidia ufyonzwaji wa vitamini muhimu.

Mafuta mazuri ni yapi?

  • Mafuta ya alizeti, ufuta, na nazi: yana asidi muhimu za mafuta.

  • Karanga, mbegu za maboga na alizeti: chanzo kizuri cha mafuta na protini.

  • Parachichi: lina mafuta ya asili yanayosaidia afya ya moyo na ubongo.

  • Samaki wa mafuta (dagaa, sato): huongeza Omega-3 kwa watoto na wazee.

Faida za mafuta mazuri kipindi cha baridi:

  • Huongeza joto la mwili.

  • Husaidia ngozi isikauke.

  • Husaidia kinga ya mwili kufanya kazi vizuri.

Angalau asilimia 20–35 ya nishati ya kila siku itokane na mafuta bora. Wazazi na walezi msisite kutumia mafuta ya asili katika maandalizi ya chakula cha familia.

 
 
 

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page