Uji wa Lishe kwa Watoto: Kinywaji Bora Kipindi cha Baridi
- ThriveCare Nutrition
- Jul 16
- 1 min read
Uji wa lishe ni mlo bora sana kwa watoto wakati wa baridi kwani hutoa nishati na virutubisho vingi kwa wakati mmoja.
Faida za uji wa lishe:
Unapasha mwili joto.
Hutoa nishati inayohitajika kwa shughuli za kila siku.
Unakuwa na virutubisho muhimu kama protini, madini na vitamini.
Ni rahisi kumezwa hata kwa watoto wadogo au wagonjwa.
Jinsi ya kuandaa uji wa lishe:
Nafaka tofauti: mtama, uwele, mahindi, na mchele.
Mbegu na karanga: mbegu za maboga, alizeti, karanga.
Viungo asilia: tangawizi kidogo kwa ladha na faida ya kiafya.
Weka mchanganyiko huu kwa uwiano sahihi, usage kwa pamoja na uchemshie kwa maji safi hadi upate uji mzito wa kuvutia. Unaweza kuongeza maziwa au nazi ili kuongeza virutubishi.
Comments