Uhusiano kati ya Lishe na Malaria kwa Watoto na Wazee
- ThriveCare Nutrition
- Apr 23
- 1 min read
Aprili 25 ni Siku ya Malaria Duniani. Ingawa lishe haiwezi kuzuia malaria moja kwa moja, inaweza kusaidia mwili wa mtoto au mzee kupambana na ugonjwa huu.
Jinsi lishe bora inavyosaidia dhidi ya malaria:
Huongeza kinga ya mwili kupambana na maambukizi.
Husaidia kupona haraka endapo mtu atapata malaria.
Vyakula vinavyopendekezwa wakati wa na baada ya malaria:
Matunda yenye vitamini C (machungwa, embe): kusaidia kinga.
Mboga za majani (mchicha, matembele): kwa ajili ya madini ya chuma.
Vyakula vya wanga (uji wa lishe, wali, viazi): kwa ajili ya nishati.
Protini (maharagwe, mayai, samaki): kusaidia ujenzi wa mwili na kupona kwa haraka.
Wizara ya Afya, inapendekeza lishe bora kama sehemu ya mkakati wa jumla wa afya kwa watu wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi ya mara kwa mara ya malaria.
Comments