Kupunguza Hatari ya Osteoporosis kwa Wazee Kupitia Lishe
- ThriveCare Nutrition
- Jul 21
- 1 min read
Osteoporosis ni hali inayosababisha mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kwa urahisi, hasa kwa wazee. Lishe bora ni nguzo muhimu ya kuzuia na kudhibiti hali hii.
Kwa nini wazee wako kwenye hatari zaidi?
Kupungua kwa homoni (hasa kwa wanawake baada ya hedhi)
Kupungua kwa ulaji wa virutubisho vinavyojenga mifupa
Kutofanya mazoezi ya viungo
Lishe bora inayosaidia mifupa kuwa imara:
Kalsiamu- Maziwa na bidhaa zake, dagaa wanaoliwa na mifupa, mboga za majani kama mchicha
Vitamini D-Samaki wa mafuta (kama sato na dagaa), mayai, na mwanga wa jua asubuhi
Magnesiamu na Fosforasi-Karanga, mbegu za alizeti, uji wa lishe, nafaka zisizokobolewa (mtama, uwele)
Protini ya kutosha- Maharagwe, maziwa, nyama isiyo na mafuta
Vidokezo vya kuzingatia:
Wazee wapewe uji wa lishe na dagaa mara kwa mara
Tumia vyakula vyenye virutubisho badala ya virutubisho vya dukani (supplements), isipokuwa kwa ushauri wa daktari
Wazee wafanye mazoezi mepesi kama kutembea au kunyoosha viungo kila siku
Kwa mujibu wa Miongozo ya Taifa ya Lishe Tanzania na WHO, ulaji wa kutosha wa kalsiamu na vitamini D hupunguza hatari ya mifupa kuporomoka kwa wazee.
Comments