Jinsi ya Kuimarisha Kinga Wakati wa Kipindi cha Baridi
- ThriveCare Nutrition
- Jun 23
- 1 min read
Kipindi cha baridi huambatana na ongezeko la magonjwa kama mafua, kikohozi na maambukizi ya njia ya hewa. Watoto na wazee wako katika hatari zaidi, hivyo ni muhimu kuwa na lishe inayosaidia kinga ya mwili.
Vyakula vinavyosaidia kuimarisha kinga:
Matunda yenye vitamini C kama mapera, machungwa, na embe – husaidia kuongeza kinga ya mwili.
Mboga za majani (mchicha, matembele) – zina vitamini A na folate kwa ulinzi wa mwili.
Samaki na maharagwe – vina protini na madini ya zinc ambayo husaidia uponaji na ukuaji wa seli mpya.
Karanga na mbegu – zina mafuta mazuri na vitamini E kwa ulinzi wa seli.
Vidokezo vya lishe kipindi cha baridi:
Kula milo mitatu kamili kwa siku na vitafunwa vyenye afya.
Tumia vinywaji vya moto kama uji, chai ya tangawizi au supu.
Punguza vinywaji baridi visivyo na virutubisho.
Kula vyakula mchanganyiko na vya asili ni njia bora ya kuimarisha kinga ya mwili kwa msimu huu.
Comments