Je, Watoto Wanaweza Kunywa Vinywaji Baridi?
- ThriveCare Nutrition
- Apr 16
- 1 min read
Vinywaji baridi vyenye sukari vinaweza kuathiri afya ya watoto ikiwa vitatumika mara kwa mara. Wazazi wengi hujiuliza ni kipi ni salama kwa watoto wao.
Madhara ya vinywaji vyenye sukari nyingi:
Huongeza hatari ya kuoza kwa meno.
Huchangia uzito kupita kiasi na hatari ya ugonjwa wa kisukari (diabetes type 2)
Hupunguza hamu ya kula chakula chenye virutubisho muhimu.
Chaguzi salama na zenye afya kwa watoto:
Maji safi na salama: Kinywaji bora zaidi kwa watoto.
Juisi asilia ya matunda (isiyoongezwa sukari): Kama juisi ya embe, nanasi au chungwa. Kunywa kwa kiasi.
Maziwa: Hutoa kalsiamu, protini na vitamini muhimu kwa watoto.
Smoothie za matunda: Zilizotengenezwa nyumbani bila sukari nyingi.
Shirika la Afya Duniani linashauri watoto kuepuka vinywaji vyenye kafeini na sukari nyingi, badala yake kupata vinywaji vyenye virutubisho vya asili vinavyochangia afya njema.
Comments